Baadhi ya vifaa vilivyochomeka. [Osman Suleiman]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mali isiyojulikana thamani imechomeka moto baada ya afisi ya mwakilishi wa walemavu kaunti ya Mombasa Ramla Salim kushika moto usiku wa kuamkia siku ya Jumapili.

Afisi hiyo ambayo iko katika jengo la shule ya msingi ya Mvita ilishika moto mwendo wa saa sita usiku wa kuamkia Jumapili.

Kulinagana na Ramla moto huo uliteketeza tarakilishi tano na vifaa vyote vinavyotumiwa kufundishia watoto walemavu.

Chanzo cha moto huo hakijabainika hadi kufikia sasa,huku uchguguzi ukiendelea.

Mwanahabari huyu, alizuru eneo hilo na kuona majivu na mabaki ya tarakilishi hizo zikiwa zimetapakaa chini.

Kulingana na mwakilishi huyo moto huo ulichukua takribani saa moja kwa wazima moto kutoka kaunti ya Mombasa pamoja na majirani kuweza kuudhibiti.