Ujenzi wa sehemu tatu za kupakulia makasha tayari umekamilika katika Bandari ya Lamu .[Picha/ constructionkenya.com]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Bandari mpya ya Lamu inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni baada ya ujenzi kukamilika katika baadhi ya sehemu za bandari hiyo.Akizungumza na wanahabari katika hoteli moja jijini Mombasa siku ya Jumatatu, mkurugenzi mkuu wa Bandari ya Mombasa Catherinne Muturi alisema kuwa sehemu tatu za kupakulia makasha zitakuwa tayari hivi karibuni, hatua inayotarajiwa kurahisisha kazi bandarini humo.“Tayari ujenzi wa sehemu tatu za kupakulia makasha unakaribia kukamilika huku zingine zaidi zikitarajiwa kujengwa hivi karibuni,” alisema Muturi.Aidha, Muturi amedokeza kuwa miundo mbinu mingine inaendelea kukarabatiwa ili kufanikisha lengo kuu la bandari hiyo.“Ukarabati bado unaendelea ili lengo kuu la bandari hii litimizwe,” alisema Muturi.Vile vile ameeleza kuwa bandari hiyo itakuwa na sehemu za kupakuwa makasha zaidi ya 50.“Tutakuwa tunapakuwa makasha zaidi ya 50 katika bandari hiyo ya kisasa ya Lamu,” alisema Muturi.Aidha, Muturi alisema kuwa watatoa taarifa kamili kuhusu ujenzi wa bandari ndogo katika Kaunti za Kwale na Kisumu baada ya ukaguzi kukamilika.