Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho na aliyekuwa Seneta wa Mombasa Hassan Omar wakiwa mahakamani [Picha | barakafm.org]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mahakama kuu ya mjini Mombasa Ijumaa inatarajiwa kuskiliza ombi la aliyekuwa Seneta wa Mombasa Hassan Omar anayetaka kuondoa kesi ya kupinga ushindi wa Gavana wa Mombasa Hassan Joho.Omar amewasilisha ombi la kuondoa kesi hiyo kwa misingi kwamba hana imani na Jaji anayeskiza kesi hiyo Lydia Achode.Ameelezea hofu kwamba huenda asipate haki kwenye kesi hiyo huku akidai Jaji Achode amekua akipendelea upande wa Gavana Joho.Omar ambaye aliwania kiti cha ugavana Mombasa kupitia chama cha Wiper halkadhalika anamlaumu Jaji kwa mapendeleo hasa baada ya kumnyima wakili wake Yusuf Aboubakar nafasi ya kumhoji Joho kuhusiana na uhalali wa vyeti vyake vya chuo kikuu.Awali Omar aliwasilisha ombi la kumtaka Jaji Achode ajiondoe kwenye kesi hiyo, ombi ambalo lilipuuziliwa mbali huku Jaji akilitaja kama lisilokuwa na msingi wowote.Kwenye kesi hiyo, Omar aliyemaliza nafasi ya tatu kwenye kinyang'anyiro cha ugavana Mombasa anataka ushindi wa Joho kubatilishwa kwa kuwa uchaguzi wa Agosti nane mwaka jana haukua wa huru na haki.Kuwa wa kwanza kujua kuhusiana na habari muhimu pindi zinapotokea. Tuma ujumbe kupitia nambari ya WhatsApp 0740950002 ukianza na mojawapo ya maneno yafuatayo ili uanze kupokea taarifa moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi: Mombasa Crime, Mombasa Breaking, Mombasa Politics.