Jaji mkuu David Maraga, viongozi wengine, mahakimu na majaji wengine.[Osman Suleiman]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Jaji mkuu nchini David Maraga amezindua rasmi ujenzi wa mahakama kuu ya  Mombasa.Mahakama hiyo itagharimu kima cha shilingi milioni 445.

Akizungumza siku ya Jumatano katika jengo la mahakama ya Mombasa, Alisema kuwa ujenzi huo unatazamaniwa kumalizika mwezi March mwaka ujao.

Jaji Maraga amesema kuwa mahakama hiyo itakuwa na chumba maalum cha kunyonyeshea watoto.Wakati huo huo amewataka wanakandarasi waliopewa ujenzi huo kuhakikisha wanaukamilisha kabla ya mwezi Machi ili wananchi waweze kupata huduma.

Huku hayo yakijiri jaji Maraga amesema idara ya mahakama  itajenga mahakama ndogo katika eneo bunge la Changamwe na Likoni iwapo serikali ya kaunti ya Mombasa itatoa vipande vya ardhi kwa ujenzo huo.

Maraga ametaja hatua ya ujenzi wa mahakama hizo itafanikisha huduma bora kwa wakazi wa maeneo hayo.

Aidh amesema kuwa wanapanga kuanzisha mahakama tamba zitakazo hudumia wananchi maeneo ya vijijini.Kauli yake inajiri baada ya chama cha mawakili kupitia mwenyekiti wao, Mathew Nyabena kupendekeza kujengwa kwa mahakama hizo,ili kuwapunguzia wakazi wa maeneo hayo gharama za usafiri.

Mathew amesema wakazi wengi wa eneo bunge la Likoni wanapata changamoto hasa katika kivuko cha Ferry, hali inayochangia wengi wao kuchelewa kuhudhuria vikao vya kesi zao.

Kwa upande wake gavana wa Mombasa Hassan Joho amesema kuwa serikali yake itatenga vipande hivyo vya ardhi kufanikishha ujenzi wa mahakama hizo ndogo.