Mbunge wa Likoni Mishi Mboko.[radiorahma.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama kuu ya Mombasa imeagiza kuhesabiwa upya kura za eneo bunge la Likoni kwenye kesi ya kupinga ushindi wa mbunge Mishi Mboko.

Hatua hii inajiri baada ya aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Masoud Mwahima kuwasilisha ombi la kutaka kuhesabiwa upya kwa kura hizo ili kubaini mshindi halali wa uchaguzi wa Agosti nane.

Mwahima anadai kulikuwa na wizi wa kura katika eneo hilo wakati wa uchaguzi wa Agosti nane mwaka jana.

Siku ya Jumanne, jaji Erick Ogola ameagiza kura hizo kuhesabiwa upya Januari 29 mwaka huu.

Mishi alikanusha madai ya kuhusika katika wizi wa kura katika eneo bunge hilo.

Akitoa ushahidi huo siku ya Jumatatu mbele ya jaji Erick Ogola wa mahakama ya Mombasa, Mishi alipinga madai kuwa kulikuwa na wizi wa kura katika vituo vya kupigia kura eneo bunge la Likoni.

Aliongeza kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa uwazi na haki na kuongeza kuwa watu wa Likoni walimchagua kwa moyo mmoja kinyume na inavyodaiwa na Mwahima.

Aidha,amepinga kuwa aliwashurutisha wasimamizi wa uchaguzi eneo bunge la Likoni ili kumtangaza mshindi kwenye uchaguzi huo kama  inavyodaiwa na Mwahima.

Mishi alisema kuwa hana ufahamu kama nguvu za umeme zilipotea wakati wa kuhesabiwa kwa kura hizo katika kituo kikuu cha kuhesabiwa kura cha Likoni school for the blind kama anavyodai Mwahima.

Ameongeza kuwa hana ufahamu wowote wa iwapo mawakala wake walishikwa na kufikishwa polisi kwa madai ya kuhusika na wizi wa kura.

Wakati huo huo amesema kuwa hana ufahamu iwapo watu walisafirishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine ili kupiga kura katika vituo vya eneo bunge la Likoni.

Miezi miwili iyopita mbunge za zamani Masoud Mwahima aliambia mahakama kuwa hakukuwa na umeme katika kituo kikuu cha kujumuisha kura cha Likoni School for the blind.

“Hakukuwa na umeme na iliwalazimu maafisa wa IEBC kutumia mwangaza wa simu kujumuisha kura hizo. Ni wazi kuwa kulishuhudiwa wizi wa kura,” alisema Mwahima.

Mwahima alidai kuwa mawakala waliohusika katika uchaguzi huo wa ubunge eneo la Likoni walikuwa bandia na wala sio wa chama cha Jubilee.

“Mawakala waliotumika kusimamia kura hawakuwa wa Jubilee wala siwajui kamwe. Hao ni mawakala bandia na walifanywa kuokotwa mitaani,” alisema Mwahima.

Mwahima alidai kuwa mawakala waliohusika katika uchaguzi huo wa ubunge eneo la Likoni walikuwa bandia na wala sio wa chama cha Jubilee.

“Mawakala waliotumika kusimamia kura hawakuwa wa Jubilee wala siwajui kamwe. Hao ni mawakala bandia na walifanywa kuokotwa mitaani,” alisema Mwahima.

Kesi ya kupinga ushindi wa Mboko iliwasilishwa mahakamani na aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Masoud Mwahima ambaye aliwania kupitia chama cha Jubilee.