Mwakilishi wa wanawake Kaunti ya Mombasa Asha Mohamed akipokea cheti chake cha ushindi. [Picha: Hassan Joho/ facebook.com]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mpiga kura Saad Yusuf Saad amekata rufaa kupinga ushindi wa mwakilishi wa wanawake Kaunti ya Mombasa Asha Mohamed.Saad amekata rufaa hiyo katika Mahakama ya Rufaa ya Malindi.Akizungumza na mwanahabari huyu, Saad alisema kuwa hakukubaliani na uamuzi uliotupilia mbali kesi hiyo.Saad alisema kuwa ana imani kuwa atapata haki yake ya kikatiba.“Nina imani ya kupata haki yangu katika Mahakama ya Rufaa,” alisema Saad.Haya yanajiri baada ya Mahakama kuu ya Mombasa kutupilia mbali kesi hiyo ya kupinga ushindi wa Mohamed.Wiki iliyopita, Jaji Thande Mugure alitupilia mbali kesi hiyo kwa kusema kuwa haikutimiza vigezo muhimu vya kesi za uchaguzi.Jaji Mugere alisema kuwa Saad alikosa kuchapisha kesi hiyo kwenye gazeti kwa mujibu wa katiba.Jaji huyo aidha alimlaumu Saad kwa kumkabidhi mtoto wa Hussein mwenye umri wa miaka minane nakala za kesi hiyo, hatua ambayo ni kinyume cha kanuni za kesi za uchaguzi.Ikumbukwe mwezi uliopita, Saad aliwasilisha ombi la kutaka jaji huyo kujiondoa kwenye kesi hiyo kwa kudai kuwa hakuwa na imani naye.Hatahivyo, Jaji Mugure alidinda kujiondoa kwenye kesi hiyo na kusema katiba inamruhusu kuisikiza.Kufikia sasa, Jaji Mugure ametupilia mbali kesi tatu za uchaguzi zilizowasilishwa mbele yake, ya hivi punde ikiwa ya kupinga ushindi wa Gavana wa Kwale Salim Mvurya.