Jengo la Mahakama ya Mombasa. [Photo/ the-star.co.ke]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mahakama ya Mombasa imemuachilia huru mshukiwa wa kundi la al-Shabaab baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.Kassim Stadi alitiwa mbaroni mnamo December 7, 2012 katika mtaa wa Mtopanga eneo bunge la Kisauni, baada ya kudaiwa kuhusika na kundi hilo la kigaidi.Aidha, Stadi anakabiliwa na shtaka ya kumiliki bunduki na risasi bila kibali kwa mujibu wa sheria.Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatano, Hakimu Francis Kyambia alisema kuwa upande wa mashtaka ulikosa kuwasilisha ushahidi wa kutosha mbele ya mahakama hiyo.Kyambia alisema kuwa ushahidi uliowasilishwa mbele yake ni hafifu mno kwa hivyo hawezi kumfunga gerezani mshukiwa huyo.“Ushahidi uliowasilishwa mbele yangu ni hafifu na hauwezi nisababisha kumfunga gerezani mshukiwa huyu,” alisema Kyambia.Aidha, Kyambia alitilia shaka bunduki na risasi zinazodaiwa kumilikiwa na mshukiwa huyo.Hakimu huyo alisema kuwa huenda bunduki hizo zilipelekwa katika makaazi ya mshukiwa huyo na maafisa wa usalama walioenda kufanya uchunguzi nyumbani humo.