Mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka saba ya wizi wa mabavu. [Photo/ shutterstock.com]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume mwenye umri wa makamo amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa mabavu.Dancan Ouma Owour alikuwa anakabiliwa na mashtaka saba ya wizi wa mabavu.Mahakama iliskia kuwa Owour alitekeleza wizi huo mnano Novemba 24, 2016 katika hoteli ya Pine Court huko Malindi.Inaripotiwa kuwa Owour na wenzake walimwibia Charles Katana bidhaa mbali mbali zenye thamani ya takrbani shilingi laki moja, huku wakiwa wamejihami kwa silaha hatari.Aidha, Owour anadaiwa kumuibia Adam Ndoro pete ya dhahabu, mikufu miwili ya shaba na simu, zote zikiwa zenye thamani ya Sh23,000.Akitoa uamuzi wake siku ya Jumanne, Hakimu mkuu mkaazi Yvonne Khatambi alisema kuwa amemhukumu Owour kifungo cha maisha ili iwe funzo kwa wengine wanaojihusisha na wizi wa mabavu.“Hii itakuwa funzo kwa wengine wanaopanga kutekeleza wizi katika eneo hili,” alisema Hakimu Khatambi.Owour ana siku 14 kukata rufaa.