Mkuu wa shirika la Muhuri Khelef Khalifa akiwahutubia wanahabari hapo awali. [Photo/ nation.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Shirika la kutetea haki za binadamu la Muhuri linataka kufidiwa Sh2,157,370 zilizotumiwa wakati wa kesi ya kufungwa kwa akaunti zao za benki mwaka 2015. Shirika hilo kupitia mwenyekiti wake Khelef Khalifa lilisema kuwa pesa hizo zitagharamia gharama iliyotumia wakati wa kesi hiyo.Muhuri imeishtaki afisi ya mkuu wa sheria, Inspekta mkuu wa polisi na benki kuu ya taifa.Khelef alisema hatua ya kufungwa kwa akaunti zao iliwafanya wafadhili wao wakuu kutoa ufadhili wao kwa shirika hilo, hali iliyosababisha ukosefu wa fedha.Kesi hiyo itatajwa Machi 3, 2018 mbele ya jaji Njoki Mwangi, ili kubaini iwapo mkuu wa sheria na inspekta generali wa polisi wamewasilisha majibu yao kuhusiana na kesi hiyo.Ikumbukwe shirika hilo pamoja na lile la Haki Afrika yalifungiwa akaunti zao za benki mwaka 2015 baada ya kuhusishwa na madai ya kufadhili ugaidi.Hatahivyo, madai hayo yalitupiliwa mbali na mahakama kuu ya Mombasa.Jaji Anyara Emukule alisema siku ya Jumanne kuwa kufungwa kwa akaunti za mashirika hayo ni kinyume na katiba.Aidha, aliongeza kuwa inspekta jenerali wa polisi alikiuka katiba kwa kuagiza kufungwa kwa akaunti hizo, kwani hana mamlaka yoyote kikatiba ikizingatiwa kuwa waziri wa usalama ndiye anao uwezo wa kuagiza kufungwa kwa akaunti hizo.Vile vile, alisisitiza kuwa inspekta jenerali hakutoa sababu za kutosha zinazohusisha mashirika hayo na ufadhili wa ugaidi.