Mwanamke mjamzito. [Picha/ modernghana.com]

Share news tips with us here at Hivisasa

Imebainika kuwa visa vya watoto kufia tumboni vinazidi kuongezeka katika kaunti ya Mombasa, Kwale na Kilifi.Kauli hii imetolewa na mwenyekiti wa idara ya afya ya uzazi katika Chuo Kikuu cha Aga Khan Profesa Marleen Temmerman.Profesa Marleen amesema hali hiyo inafaa kukabiliwa ili kupunguza vifo hivyo katika kaunti hizo tatu.Aidha, ameongeza kuwa idadi ya watoto wengi hufariki baada ya kuzaliwa hali inayovunja moyo wazazi.Akizungumza siku ya Alhamisi katika warsha iliyowaleta pamoja watafiti mbalimbali kutoka idara ya afya kutoka Uchina na vyuo vikuu barani Afrika, Temmerman alisema licha ya ongezeko la idadi hiyo ya vifo vya watoto, visa vya kina mama kufa wakiwa wajawazito vimepungua.“Idadi ya wanawake wanaofariki wakiwa na ujauzito imepungua kote nchini kwani wanawake wameanza kuzingatia maagizo ya madaktari,” alisema Temmerman. Aidha, ameeleza kuwa katika kukabiliana na tatizo hilo, kuna haja ya kuboreshwa kwa miundo msingi sambamba na huduma za matibabu.Kwa upande wake, Dkt Robert Armstrong alisema kuwa ushirikiano wao unalenga kubaini matatizo yanayokumba mataifa ya Bara Afrika haswa Afrika Mashariki ili kuwasaidia wananchi.Kuwa wa kwanza kujua kuhusiana na habari muhimu pindi zinapotokea. Tuma ujumbe kupitia nambari ya WhatsApp 0740950002 ukianza na mojawapo ya maneno yafuatayo ili uanze kupokea taarifa moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi: Mombasa Crime, Mombasa Politics, Mombasa Sports, Mombasa Agriculture, Mombasa Random, Mombasa Health, Mombasa Business, Mombasa Environment, Mombasa Entertainment, Mombasa Transport, Mombasa Opinion, Mombasa Education.