Walinzi wa Slovit Security Guards.[Osman Suleiman]

Share news tips with us here at Hivisasa

Walinzi wawili kampuni ya ulinzi ya Solvit Security Guards watazuiliwa kwa muda wa siku tano zaidi katika kituo cha polisi cha Bamburi baada ya kuhusika katika mauwaji ya mfanyikazi wa benk ya Stanbic.

Hamisi Karisa na Said Mwalungo wanadaiwa kumuuwa David Kamau katika eneo la Nyali Centre mnamo Januari 7,2018.

Washukiwa hao wanadaiwa kumshambulia mwendazake na kumjeruhi hali iliyosababisha kifo chake.

Wawili hao hawakusomewa mashtaka siku ya Alhamisi baada ya afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kuomba washukiwa hao kuzuiliwa kwa siku tano wakisubiri uchunguzi kukamilika.

Mwendesha mashtaka Erick Masila aliambia mahakama kuwa wawili hao wanafaa kuchukuliwa alama za vidole pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa akili katika hospitali ya Makadara jijini Mombasa.

Masila alimwambia jaji Dora Chepkwonyi kuagiza kuzuiliwa kwa wawili hao katika kituo cha polisi cha  Bamburi.

Kesi hiyo itatajwa Januari 31,2018.