Mbunge wa Nyali Mohamed Ali anamlaumu Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho kwa kusambaratika kwa uhusiano miongoni mwa wabunge eneo la Pwani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na Ali, Joho anatumia wadhifa wake ndani ya chama cha ODM kunyanyasa wabunge waliochaguliwa kupitia chama hicho. 

"Baadhi ya wabunge wanatishiwa kung’atuka kutoka chama hicho hatua ambayo itawapelekea kupoteza viti vyao," alisema Ali katika hafla ya kuanzisha mfumo wa kuwapa wanafunzi wa Nyali hela za 'bursary' shilingi milioni 30 za Kenya, Februari 16.

Kulingana na mbunge Ali, Joho yuatumia vibaya mamlaka yake kwenye kaunti na kwenye ODM.

Haya yanajiri baada ODM kupendekeza kutimuliwa kwa wabunge Aisha Jumwa wa Malindi na Suleiman Dori wa Msambweni kutoka chamani kufuatia uhusiano wao wa kisiasa naye Naibu wa Rais William Ruto.

Jumwa anamlaumu Joho na kudai kuwa ndiye chanzo cha matatizo anayoyapitia chamani.

#hivisasaoriginal