Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kisii, John Akama, amesema huenda mkataba ukawekwa hivi karibuni kuwezesha chuo hicho kupata ufadhili wa kufanikisha taaluma mpya ulioanzishwa chuoni humo almaarufu kama 'e-waste management'.

Akihutubu katika hafla ya kukaribisha viongozi kutoka Benki Kuu ya Dunia chuoni humo siku ya Jumanne, Prof Akama alisema kuwa wanamipango ya kuwa makao makuu ya taaluma hiyo nchini na hata barani Afrika pindi tu mkataba wa maelewano utakaohidhinishwa rasmi.

“Ni wazi kuwa Chuo Kikuu cha Kisii ni moja kati ya vyuo vya masomo ya juu vinavyo kuwa kwa kasi sana. Chuo hiki kinatarajia kuanzisha taaluma ya 'e-waste management' ambayo itakuwa ya kwanza nchini jambo ambalo tunalijivunia zaidi,” alisema Akama.

Aidha Prof Akama aliongeza kuwa wangependelea kuwa na makubaliano na benki hiyo ya dunia ili kufadhili baadhi ya miradi iliyoanzishwa na chuo hicho.

“Tunafurahia kuwa ujumbe maalum kutoka Benki Kuu ya Dunia wanania ya kusaidia chuo chetu. Lengo lao ni kuona kwamba mazingira ya masomo ni bora zaidi inavyopaswa,” aliongeza Akama.

Baadhi ya wanafunzi tuliozungumza nao wameeleza furaha yao hasa wanapotarajia kuona sura mpya ya chuo hicho pindi tu mkataba wa maelewano utakaohidhinishwa rasmi.

“Tunafurahia hatua iliyopigwa na uongozi wa chuo hiki kwani inapania kuboresha mazingira ya masomo chuoni, sio tu katika taaluma mpya inayoanzishwa bali katika sekta zote chuoni. Kama kiongozi wa wanafunzi nimefurahishwa na hatua hii,” alisema Jeff Mitei.