Jengo la mahakama ya Mombasa. [Picha/Haramo]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kesi ya waathiriwa wa sumu ya Lead kutoka eneo la Changamwe imeahirishwa katika mahakama kuu ya Mombasa.

Kesi hiyo imeahirishwa baada ya wahusika wakuu wa kampuni ya Kenya Metal Refinery, kukosa kufika mahakamani bila sababu mwafaka siku ya Jumatatu.

Jaji Ann Omollo amesema ameamua kuaharisha kesi hiyo ili kutoa fursa kwa pande zote mbili kupatikana mahakmani kwa ajili ya usawa na uwazi.

Ikumbukwe kuwa kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na Kevin Musyoka na wengine tisa mnamo Februari 20,2016, baada ya wakaazi takriban elefu tatu kutoka kijiji hicho kauathiriwa na sumu ya Lead kutoka kwa kampuni ya  Kenya Metal Refinery mnamo mwaka 2009.

Waathiriwa hao wanailaumu serikali na kampuni hiyo kwa utepetevu katika kulinda mazingira na afya ya jamii pamoja na kutaka kufidiwa kwa maafa yaliwakumbuka.

Zaidi ya wakazi 3,000 wanataka kufidiwa shilingi bilioni 1.6 ili kukidhi mahitaji yao ya matibabu pamoja na kufidiwa waliofariki kutokana na sumu hiyo.

Zaidi ya nyumba 580 za wakazi hao zimeathirika na sumu hiyo ya Lead.