Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Masaba kaunti ya Kisii Elijah Moindi amewaomba vijana wote katika eneo bunge hilo kutokubali kutumika vibaya na wanasiasa na badala yake kutafuta la kufanya ili kujisaidia siku zijazo.

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa baadhi ya vijana hutumikia vibaya na wanasiasa jambo ambalo limeongeza ukosefu wa maendeleo katika sehemu mbalimbali za eneo bunge hilo.

“Naomba vijana wa eneo bunge langu lote kujihusisha kwa masuala ambayo yatawasaidia katika siku zijazo badala ya kutumika vibaya na wanasiasa ambao wanaendesha siasa ambazo hazina maendeleo,” alisema Moindi.

Moindi aliwaonya vijana ambao hukaa kando kando ya barabara wakisubiri viongozi kupita ili kuwapokeza pesa kwa kuwaomba wajiunge kwenye vikundi ndiposa wapate pesa za mikopo kutoka kwa serikali zitakazo wawezesha kufanya biashara na kujiendeleza.