Share news tips with us here at Hivisasa

Naibu mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC Lilian Mahiri amesema tume hiyo imewaajiri wataalum katika idara ya teknolojia na mawasiliano ICT ili kuona kuwa vifaa vya kielektroniki vya kuwasajili wapiga kura vinafanya kazi ipasavyo.

Katika kikao na wanahabari jijini Kisumu, Mahiri alisema hatua hiyo inapania kuona kuwa vifaa hivyo havifeli kama ilivyoshuhudiwa kwenye uchaguzi uliopita.

‘’Naomba msisahau kuwa hizi ni mashine tu ambazo zinastahili kudhibitiwa na ndio sababu tumeweka maafisa wataalamu katika maswala na mawasiliano kudhibiti hali mapema ndiposa tusishuhudie changamoto baadae,’’ Mahiri alsiema.

Ametoa wito kwa wale ambao hawajajiandikisha kama wapiga kura kuhakikisha kuwa wanajisajili mapema ili kuzuia msongamano nyakati za mwisho.

Mahiri alisisitiza umuhimu wa washikadau wote katika uchaguzi kushirikiana ili kufanikisha zoezi hilo.