Vikundi vya vijana wanaorandaranda nyakati za usiku na alfajiri vimehusihwa pakubwa na uporaji wa mali katika vituo vya mabasi ya kuelekea mjini Nairobi hapa Mombasa.
Kulingana na wahudumu wa kampuni za mabasi katika eneo la maegesho, Mwembe Tayari.
Vikundi vya vijana huzurura nyakati za alfajiri na usiku na kuwapora wasafiri huku wengine wakivunja hata vioo vya magari ya kibinafsi yanayoegeshwa katika eneo hilo.
Aidha wahudumu hao wamesema kwamba usalama wa eneo hilo umedorora kwa kiasi kikubwa kwani kwa sasa vijana hao wamejua muda ambao askari hufika eneo hilo.