Share news tips with us here at Hivisasa

Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa amewahakikishia watalii usalama wao.

Marwa aliwahakikishia watalii wenye mpango wa kuzuru Mombasa msimu huu wa likizo kwamba idara ya polisi imeweka usalama wa kutosha.

Akizungumza na wanahabari katika ufuo wa bahari wa Jomo Kenyatta maarufu kama Pirates Beach Mombasa siku ya Jumatatu, Marwa alitoa onyo kwa wale wenye nia ya kuvuruga usalama kwa kusema kwamba serikali iko macho.

“Ningependa kuchukua fursa hii kuwaalika watalii Mombasa. Kuna amani kila sehemu hata kwenye kivuko cha ferry, uwanja wa ndege na maeneo yote ambayo huwa yanashuhudia watu wengi msimu huu. Tumeimarisha usalama katika kaunti hii,” alisema Marwa.

Marwa alisema kuwa tayari sehemu maalum imetengwa katika ufu huo ambapo maafisa wa usalama wanatarajiwa kukita kambi watakapokuwa wakishika doria.