Mtihani wa kidato cha nne ukiwa tayari umetangazwa siku ya Alhamisi na kila shule pamoja na watahiniwa kujua hatima yao.
Wazazi katika Kaunti ya Mombasa wamepongeza baadhi ya shule kutoka Kaunti hiyo kwa kuiweka kwenye ramani ya taifa kwa kuwa na matokeo mazuri kwenye mtihani wa mwaka jana.
Akiongea na kwa niaba ya wazazi wengine pindi tu baada ya waziri wa elimu Matiang’i kutangaza mtihani huo, Rukiya Hussein mmojawepo wa wazazi alisema kuwa wanafunzi hao waliofanya vizuri wanahitaji pongezi.
Ikizingatiwa kuwa, wengi wao walikuwa nje kwa zaidi ya wiki tano, kufuatia mgomo wa walimu ambao ulilemaza shughuli za masomo nchi.
"Tuna furaha kwa baadhi ya shule zetu kufanya vyema kwenye mtihani wa mwaka jana ni furaha yetu kama wazazi na jamii nzima ya eneo la Mombasa," alisema Hussein.
Baadhi ya shule ambazo zilibobea kwenye mtihani huo ni pamoja na shule ya Sheikh Khalifa Bin Zayed, Mombasa Lights academy, Istqama Schools, shule ya wasichana ya Coast miongoni mwa nyingine ambazo ziliweka rekodi nzuri ikilinganishwa na miaka nyuma.
Takriban wanafunzi elfu 5 hawatapata matokeo yao kwa madai ya kuhusika kwenye visa vya udanganyifu ambapo Kaunti 46 zilipata magao wa udanganyifu huo ila tu Kaunti moja Isiolo ambayo haikuhusika kwenye kisa hata kimoja.