Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Huku zikisalia siku tano kabla ya uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Malindi kufanyika, viongozi mbalimbali wa kisiasa waliokita kambi katika eneo bunge hilo wakiwapigia debe viongozi wenza sasa washinikiza wakazi kuchagua kiongozi wala sio chama.

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kilifi Aisha Jumwa alisema kuwa kiongozi anaweza kuunganisha wakazi na kufanya maendeleo kwa jamii ndiye kiongozi anafaa kuchaguliwa katika kinyang’anyiro hicho.

Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa siku ya Alhamisi baada ya mkutano na makundi ya akina mama Aisha alisema kuwa wakati umefika sasa kwa wananchi kujihusisha kikamilifu katika maswala ya uchaguzi na kuwachaguzi viongozi waadilifu.

Akiongekana kumpigia debe mgombea wa kiti hicho cha eneo bunge la Malindi kupitia chama cha ODM Willy Baraka Mtengo, Aisha alisema kuwa kiongozi huyo ni mwadilifu na iwapo wakazi wa Malindi watamchagua katika uchaguzi huo mdogo, basi maswala mengi ya kimaendeleo yatatekelezwa zaidi.

"Ndugu zanguni nawaambia kuwa wakati umefika sasa kwa wananchi kuwa makini na kuwaangalia viongozi wanakuja kwao kuomba kura ni waina gani kwani viongozi wazembe hawawezi tekelezea wananchi miradi yoyote,” alisema Aisha.

Uchaguzi huo mdogo wa Malindi unatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu tarehe 7 Machi mwaka huu kujaza nafasi ya Dan Kazungu aliyeteuliwa kuwa waziri wa madini nchini.