Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Serikali ya kaunti ya Nyamira imeombwa kukarabati barabara zote ambazo ziko chini ya uongozi wa kaunti ili kurahisisha sekta ya uchukuzi katika kaunti hiyo.

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa nyingi ya barabara za kaunti hiyo bado hasijakarabatiwa jambo ambalo limeathiri sekta ya uchukuzi pakubwa.

Akizungumza siku ya Jumapili katika eneo bunge lake la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira mbunge wa eneo hilo Timothy Bosire aliomba serikali ya kaunti ya Nyamira kuhakikisha barabara zote zilizo chini ya uongozi wa kaunti zimekarabatiwa kikamilifu kabla ya uchaguzi ujao ili kuboresha sekta ya uchukuzi

“Serikali za kaunti hupokea pesa kutoka serikali ya kitaifa ambazo ni za kukarabati barabara nashangaa sana wakati ninaona barabara za kaunti hii zikiwa katika hali mbaya,” Bosire.

“Naomba gavana wa kaunti hii John Nyagarama kuhakisha barabara ambazo ni za kaunti zimekarabatiwa ili maendeleo yaonekana,” aliongeza Bosire.

Wakati huo huo, Bosire aliomba viongozi wote kufanya maendeleo katika eneo wanalowakilisha ili kunufaisha wakazi kimaendeleo.

Kulingana na Bosire viongozi huchaguliwa ili kufanya maendeleo na kusema maendeleo yanafaa kupewa kipaumbele katika kila eneo bunge nchini.