Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwakilishi wa wadi ya Sensi eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini Onchong’a Nyagaka amehimizwa kuwasilisha orodha ya wanafunzi wote waliofadhiliwa pesa za 'basari' katika wadi hiyo.

Ombi hilo limetolewa ili kuonyesha uwazi wa jinsi pesa hizo ziligawanywa kwa wanafunzi wa wadi hiyo huku ikidaiwa kua pesa hizo za 'basari' zilitolewa kwa njia ya mapendeleo.

Akizungumza nasi siku ya Jumapili mwanasiasa wa wadi hiyo Paul Angwenyi aliomba orodha ya wanafunzi waliofaidika kwa mgao huo itolewe kwa minajili ya uwazi.

Kulingana na Angwenyi kuna sehemu nyingi ambazo wanafunzi hawakufaidika hata mmoja na kudai kulikuwa na mapendeleo kwa sehemu zingine.

“Tunaomba Mwakilishi Onchong’a kuwa, wakati pesa hizo zinagawanywa sehemu zote ziwe zinafaidika maana wadi hii ni moja,” alisema Angwenyi.

Juhudi za kumtafuta mwakilishi huyo zilifua dafu naye akakukanusha madai hayo ya mapendeleo na kusema wanafunzi waliopata pesa hizo wanatoka katika sehemu zote za wadi hiyo

Sasa mwakilishi huyo anahitajika kutoa orodha kamili ili yale anayozungumza kuonekana wasi kwa wakazi wa wadi hiyo ya sensi.