Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Waziri wa usalama Joseph Nkaisery amemtahadharisha Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Ali Joho dhidi ya kujibizana na maafisa wa usalama katika vyombo vya habari na badala yake kumtaka kufuata utaratibu katika kuwasilisha malalamishi yake.

Nkaiserry amesema kuwa malumbano hayo si sawa kwa viongozi kwani huenda ikaonekana kuwa hawana nia ya kuwahudumia wananchi ila tu kujinufaisha kibinafsi.

Hii ni kufuatia uhasama baina ya gavana huyo na Kamishina wa kanda za Pwani Nelson Marwa kudhihirika wazi na viongozi hao kuonekana katika hadhara ya watu wakirushiana cheche za maneno.

Gavana huyo ameonyesha hali yake ya kutoridhika jinsi Marwa anatekeleza utendakazi wake na kulalamikia kuondolewa kazini kwa walinzi wake huku akisema kuwa maisha yake sasa yamo hatarini.