Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwenyekiti wa maktaba nchini Samuel Nyangeso ameahidi kujenga maktaba katika Wadi ya Nyatieko, eneo bunge la Kitutu Chache ili kuinua viwango vya elimu katika wadi hiyo.

Nyangeso alisema sharti viwango vya elimu viinuliwe kupitia ujenzi wa maktaba ili wanafunzi wapate fursa ya kudurusu vitabu hivyo na kupata maarifa itakayowawezesha kupita mitihani ya kitaifa.

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatatu mjini Kisii, Nyangeso alisema atajenga maktaba hiyo kwanzia mwaka ujao.

Wakati huo huo, Nyangeso aliomba viongozi katika Kaunti ya Kisii kushirikiana naye katika ujenzi wa maktaba hiyo kwa kutoa msaada ili kuinua sekta ya elimu katika kaunti hiyo.

“Nitajenga maktaba katika Wadi ya Nyatieko ili kuwapa wanafunzi mazingira bora ya kusoma na kupata maarifa,” alisema Nyangeso.

Aliongeza, “Naomba viongozi katika kaunti ya Kisii kushirikiana nami tujenge maktaba hiyo kama njia moja ya kuinua viwango vya elimu.”

Aidha, aliahidi kufadhili shule za msingi za Riangoko, Riamochogoria, Iranda na Nyatieko vitabu vya kusoma.