Afisa mmoja wa polisi amekiri kuwa gari ambalo liliwaua vijana watano katika eneo la Salgaa mkesha wa mwaka mpya lilikuwa lake.
Inadaiwa afisa huyo alikuwa amewakodisha vijana hao wa umri wa chini gari lake ambapo ni kinyume cha sheria.
Julius Kioko, ambaye ni afisa wa polisi wa utawala, alisema kuwa vijana hao walikuwa wanatumia gari lake lakini akadai kuwa ni rafiki yake aliyewapa.
“Nilimpa rafiki yangu gari kitu saa mbili hivi mkesha wa mwaka mpya lakini nilishtuka asubuhi nilipogundua lilihusika katika ajali siku iliyofuata,” alisema Kioko.
Akielezea kuhusu tukio hilo, OCPD wa Rongai Joseph Mwamburi alisema vijana hao walikuwa wa umri wa chini.
Vijana watatu ambao walikuwa pia wakisafiri kwenye gari hilo waliponea kifo kwenye ajali hiyo.