Share news tips with us here at Hivisasa

Wafanyibiashara mjini Kisii wameomba benki zote nchini kupunguza riba za mikopo ili kuwawezesha kukopa pesa kufanyia biashara zao.

Ombi hilo limetolewa baada ya riba ambayo benki hutoza wakopaji kuwa ya juu zaidi huku wafanyibiashara wakisema kuwa imekuwa vigumu kwao kukopa kwani wao hupata faida ndogo ambayo huenda ikamezwa na riba hiyo.

Wafanyibiashara hao wakiongozwa na Julius Sang’anyi na Jane Maina waliomba benki kuwapunguzia riba za mikopo ili waweze kukopa kutoka kwa benki .

“Sisi wafanyibiashara huwa tunahitaji pesa ambazo zitatuinulia biashara zetu haswa kutoka kwa benki tofauti tofauti lakini riba ambayo tunaambiwa tulipe ni ya juu zaidi,” alisema Sang’anyi.

“Tunaomba riba hiyo ipunguzwe ili tunapofanya biashara, nasi tupate kitu cha kujiendeleza kimaisha kupitia mikopo hiyo,” aliongeza Maina.