Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwakilishi wa wadi ya Bogichora kaunti ya Nyamira Beauttah Omanga ameomba serikali ya kitaifa kufidia familia ambazo zilipoteza wapendwa katika nchi ya Somalia walipokuwa wakikabiliana na wanamgambo wa Al Shabab.

Akizungumza siku ya Jumanne katika hafla ya mazishi ya mwanajeshi aliyeuawa kupitia shambulizi hilo, Omanga aliomba serikali kuhakikisha familia hizo zilizopoteza wapendwa wao zinafidiwa.

"Idadi kubwa ya wanajeshi walioshambuliwa na kuawa nchini Somalia walikuwa tegemeo katika familia zao, hali ambayo imewaacha katika hali ya ufukara naomba serikiali kuwafidia ili nao wajiendeleze,” alisema Omanga.

Wakati huo huo, wakili Steve Mogaka aliyehudhuria sherehe hiyo aliomba serikali kufahamisha famila zote zilizoadhirika kwani kuna kufikia sasa kuna wengine ambao bado hawajapata habari kuhusu hatima ya wapendwa wao.