Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa eneo bunge la Malindi wamejitokeza kwa wingi kwenye shughuli ya uchaguzi mdogo wa eneo hilo kumchagua kiongozi wanayemuenzi kujaza nafasi ya Dan Kazungu aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Madini.

Kulingana na waangalizi wa shughuli hiyo,  iwapo hali ya usalama itaendelea kuimarika, basi zoezi hilo litafanyika bila tashwishi licha ya kuwepo na tetesi kuwa kuna baadhi ya viongozi wanawalaghai wakazi kwa kuwahonga ili kuwachagua wafuasi wao.

Maafisa hao kutoka mashirika ya utetezi wa kibaidamu wakiongozwa na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Haki Afrika Hussein Khalid amesema kuwa maafisa wa tume hiyo wako macho kuhakikisha kuwa shughuli haikumbwi na udanganyifu.

“Tumeona idadi ya wapiga kura ikiwa katika foleni ndefu sana na wakazi wamejitokeza kwa wingi kupiga kura, ishara kamili kuwa wanataka kiongozi atakayeleta mabadiliko katika eneo bunge la Malindi, ila nawaomba maafisa wa usalama waendeleza kuimarisha usalama zaidi,” alieza Khalid.

Matokeo ya shughuli hiyo ya upigaji kura yanatarajiwa kutanga baada ya vituo vyote kufungwa jioni ya leo na kuahesabiwa.