Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Idara ya usalama katika eneo zima la Pwani imewahakikisha wakazi wa eneo bunge la Malindi kuwepo na usalama dhabiti wakati wa uchaguzi mdogo wa eneo Bunge la Malindi.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Kamanda mkuu wa Polisi Francis Wanjohi alisema kuwa tayari maafisa wa polisi zaidi wametumwa kushika doria eneo hilo ili kuhakikisha kuwa usalama unaimarishwa na shughuli ya upigaji kura inafanyika vyema.

Wanjohi amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa amani kwani maafisa hao wa polisi watahakikisha kuwa hakuna mtu anayetatiza shughuli hiyo, na kuwataka wakazi kuondoa hofu ya kushuhudiwa vurugu.

“Tunawahakikisha wakazi kuwepo kwa usalama dhabiti kwani maafisa wetu wa polisi wametuma Malindi kushika doria na waaazi wajitokeze kwa shughuli hiyo ya upigaji kura na kufanya zoezi hilo kumaliza mapema," alisema Wanjohi.

Wakati uo huo amewaonya vijana wanaopanga kuzua vurugu na kutatiza shughuli hiyo ya upigaji kura wa uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Malindi kuwa watakabiliwa kisheria kwani lazima swala la amani kuzingatia," aliongeza afisa huyo.

Shughuli hiyo ya upigaji kura katika eneo hilo la Malindi ni lakumchagua atakayeziba nafasi iliyowachwa wazi na Dan Kazungu aliyeteuliwa wadhfa wa Waziri wa Madini nchini.

Kamanda mkuu wa polisi eneo la pwani Francis Wanjohi. Amewahakikishia wakaazi wa eneo la Malindi usalama dhabiti wakati wa upigaji kura kwenye uchaguzi mdogo wa Malindi.