Meneja wa Kampuni ya Sukari ya Ramisi iliyoko Kaunti ya Kwale Patrick Chebosi, na wafanyikazi wengine wanne wamehukumiwa kifungo cha miezi mitatu gerezani.
Watano hao walifungwa kwa kosa la kuwazuia maafisa wa uhamiaji kuwakamata raia wa nchi ya India waliokuwa wakifanya kazi katika kampuni hiyo.
Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatatu katika mahakama ya Mombasa, Hakimu Diana Mochache aliwataka washtakiwa hao kutumikia kifungo hicho ama kutoa faini ya shilingi elfu kumi kila mmoja.
Chibosi na wenziwe wanadaiwa kuwa mnamo Oktoba 27, 2015 waliwazuia maafisa kutoka idara ya uhamiaji kutekeleza kazi yao ya kuwakamata na kuwahoji raia wa India wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ya sukari.