Share news tips with us here at Hivisasa

Rais Uhuru Kenyatta amewaonya wakaazi wa Mombasa dhidi ya kuwachagua viongozi wanaoendeleza siasa za kikabila.

Akizungumza katika soko kuu la Kongowea siku ya Jumanne, Rais Kenyatta alisisitiza umuhimu wa kudumisha umoja miongoni mwa Wakenya.

"Ningependa kuwaomba wakaazi kuasi viongozi wanaoendeleza siasa za kuwatenganisha Wakenya. Viongozi wanaoendeleza siasa za kikabila wanafaa kupuuzwa na kutofuatwa kamwe," alisema Rais Kenyatta

Aidha, ametaka hatua za kisheria kuchukuliwa kwa viongozi watakaopatikana wakiendeleza ukabila nchini.

Raisi amewataka Wakenya kuishi kwa amani na udugu ili kukuza umoja na maendeleo wa taifa.