Viongozi mbalimbali wa mrengo wa Cord kutoka Kaunti ya Mombasa wakiongozwa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho wanatarajiwa kuandaa karamu mjini Mombasa siku ya Jumatano kusherehekea ushindi wa muungano huo huko Malindi.
Hii ni baada ya aliyekuwa muwaniaji wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la Malindi kwa tiketi ya ODM Willy Mtengo, kuteuliwa kama mbunge.
Viongozi hao wanatarajiwa kuanza msafara wao mjini Malindi na kuwashukuru wakazi kwa kukiregesha kiti hicho kwa ODM, baada ya aliyekuwa Mbunge wa Malindi Dan Kazungu kuteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta kuwa waizri wa madini nchini.
Viongozi hao walisema kuwa ushindi wa Willy Mtengo kwa takriban elfu kumi na tano ni ishara kwamba bado eneo zima la Pwani limedumisha uhusiano mwema na chama cha ODM na kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao watavinyakua viti hivyo.