Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mchungaji wa Chuo Kikuu cha Kisii ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha kupambana na dawa za kulevya katika Kaunti ya Kisii kasisi Lawrence Nyaanga amewaonya wakaazi dhidi ya kuuza pombe haramu karibu na shule.

Nyaanga alisema kuwa watakaopatikana watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Haya yanajiri baada ya kubainika kuwa wagema wanaoishi karibu na shule mbalimbali huwauzia wanafunzi pombe hiyo haramu na kuathiri masomo yao.

Nyaanga alisema kuwa eneo ambazo zimeathirika zaidi ni Nyaiguta, Nyanderema na Boronyi.

Akizungumza siku ya Jumapili mjini Kisii, Nyaanga aliomba wakaazi kutoa ripoti kwa polisi wanapomfumania mgema yeyote akiuza pombe haramu, hasa karibu na shule.

Alisema kuwa watakaopatikana watakuwa funzo kwa wale ambao hufanya shughuli hiyo kisiri.

Nawaomba wagema kuasi biashara hiyo kwani pombe ilipigwa marufuku, na yeyote atakayefumaniwa akijihusiha katika biashara hiyo atachukuliwa hatua za kisheria

“Tumefanya uchunguzi na kubaini kuwa kuna baadhi ya wagema ambao hufanya biashara yao karibu na shule,” alisema Nyaanga.

Aidha, Nyaanga aliomba maafisa wa polisi kuendelea kuwasaka wale wanaoendeleza biashara hiyo.