Wakaazi wa eneo la Nyanchwa, Kisii wamefanya maandamano hadi katika afisi za gavana wa kaunti James Ongwae kwa madai ya kufungiwa barabara ya Erera-Ekemonga wanayoitumia kila siku kufika katika mji wa kisii.
Wakaazi hao waliokuwa wamebeba matawi na kuimba nyimbo za huzuni, wanasema kuwa barabara hiyo ambayo hutumiwa na wanafunzi wanaoenda shuleni katika mji wa Kisii imefungwa kwa wiki mbili sasa.
Wameandamana wakidai kuwa wanafunzi wanatembea mwendo marefu ili kufika shuleni hivyo basi kuwachelewesha.Walimtaka gavana wa kaunti hiyo kuwahutubia naye akafanya hivyo huku akiwapa uhakikisho kuwa tatizo hilo litapata suluhu.
“Niliambiwa maneno haya na Monyenye ambaye ni mwakilishi wa wadi yenu wiki jana, akaniambia kwamba watu wa Gofu wamefunga hiyo barabara na mimi niliwaita wasimamizi wa kilabu hicho ambao nitakutana nao wiki hii. Nataka nyini mnipate watu watano tunde jopo na tumalize tatizo hili kwa dakika moja,” alisema Ongwae.