Wakazi wa Kaunti ya Mombasa wamejitokeza kwa wingi kwenye msafara wa viongozi wa Cord kutoka eneo la Pwani uliofika mjini Mombasa kutoka Malindi.
Msafara huo ulioongozwa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho siku ya Jumatano ulikuwa wa kuwapongeza wakazi wa Malindi na Pwani kwa jumla, kwa ushirikiano walioonyesha tarehe saba mwezi Machi, walipokuwa wakipiga kura kumchagua mbunge atakayejaza nafasi iliyoachwa wazi na Dan Kazungu, aliyeteuliwa kama waziri wa madini.
Akiwahutubia wakazi wa Mombasa, Joho alielezea furaha yake baada ya mgombea wa Cord Willy Mtengo kutangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho, na kuwashukuru wakazi kwa kuunga mkono muungano huo.