Wakazi walio na matatizo ya macho katika eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini kaunti ya Kisii wameombwa kujitokeza na kufika katika hospitali ya Marani siku ya Jumapili tarehe ili kupimwa na kutibiwa bila malipo.
Wito huo umetolea baada ya kubainika kuwa idadi nyingi ya wakazi walio katika sehemu za mashinani hawaendi hospitali kupimwa macho wanapopata shida ya macho ikilinganiswhwa na wakazi wanaoishi karibu na mijini.
Akizumgumza siku ya Alhamisi mjini kisii waziri wa afya ktika kaunti ya kisii Sarah Omache alisema chama cha Kisii Lions Club kwa ushirikiano na Kisii Eye Hospital kitaandaa kambi ya kupima macho katika hospitali ya Marani iliyoko eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini ili kupima na kutibu wenye shida ya macho.
“Siku ya jumapili tutakuwa katika hospitali ya Marani kupima wenye shida ya macho na watatibiwa bila malipo lakini wale watakaopatikana na shida ambayo imekolea zaidi watasafirishwa katika hospitali ya Rufaa na Mafuzo mjini Kisii ili kufanyiwa upasuaji,” alisema Omache .
“Naomba wakazi wa eneo hili wenye wamekumbwa na shida hiyo waje ili wapimwe kujua hali zao,” aliongeza omache.