Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wanahabari wametakiwa kuwa waangalifu katika kulinda usalama wao wakati wa uchaguzi mdogo wa Malindi.

Kwenye kikao na wanahabari katika kituo kikuu cha kuhesabia matokeo ya uchaguzi katika shule ya upili ya Barani siku ya Jumapili, mshirkishi wa tume ya uchaguzi kanda ya Pwani Kaskazini Amina Soud, amewataka wanahabari kuwa wangalifu wakati wanapokuwa kazini.

Amesema kuwa lazima wanahabari wazingatie usalama wao kwanza kabla kwa kuhakikisha kwamba hawafika sehemu ambazo maafisa wa polisi wameshauri kuwa huenda kukawa na purukushani.

Hata hivyo maafisa wa polisi wanaendelea kushika doria katika maeneo mbalimbali ya eneo bunge la Malindi huku pia jeshi la Kenya likiwa ange kwenye vizuizi vya kuingia katika kaunti ya Kilifi hasa mji wa Malindi.

Zaidi ya wapiga kura elfu hamsini wataanza kupiga kura leo alfajiri hadi mwendo wa saa kumi na moja jioni.

Wakazi hao wanamchagua, mjumbe atakayewawakilishi katika bunge la kitaifa baada ya mbunge wao Dan Kazungu kupandishwa daraja na kuwa waziri wa madini.

Jumla ya wagombea 7 wameorodheshwa na tume hiyo ya IEBC, lakini wawili kati yao tayari wamejiondoa ingawaje majina yao bado yatakuwepo katika karatasi za kupigia kura ikizingatiwa walijitoa kuchelewa.