Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wanawake wa Mombasa wamepongeza kurudishwa kazini kwa aliyekuwa mkurugenzi mkuu katika kampuni ya mafuta nchini (National oil co-operation) Sumaiya Athman.

Wamesema kuwa jambo hilo linaonyesha mfano bora hasa kwa viongozi wanawake ambao idadi yao ni ndogo mno katika serikali.

Yusra Mohamed, mkazi wa Mtopanga alisema siku ya Jumanne kuwa hatua hiyo imeonyesha ushindi mkubwa kwa wanawake nchini.

Aidha, aliongeza kuwa wanawake hawatakubali kamwe kuona wenzao wanakandamizwa bila sababu za maana.

Naibu wa Rais William Ruto, katika kikao na viongozi wa dini ya kiislamu mapema siku ya Jumanne huko Malindi amesema Athmani atarudishwa kazini huku uchunguzi ukiendelea kufanywa.

Sumaiya alisimamishwa kazi na bodi ya kampuni hiyo baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa kumpuni hiyo alipokuwa mkurugenzi mkuu.

Akijitetea, Bi Athmani alisema kampuni hiyo imepata faida mara tatu zaidi, na kuongezeka zaidi ya mara mbili kwa rasilimali za kampuni hiyo kwa kipindi cha miaka mitano aliyokuwa mkuu wa wake.