Wasiwasi umekumba Kaunti ya Nakuru na viunga vyake baada ya kuripotiwa kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu.
Watu kadhaa eneo la Mogotio walifikishwa hospitali Jumanne na kuongeza idadi ya watu waliokuwa wameripotiwa kuugua Kipindupindu.
Mkuu wa afya kaunti ya Nakuru Samuel King’ori amesema serikali ya kaunti inajaribu kudhibiti ugonjwa huo usienee zaidi.
"Tunaweka mikakati kuhakikisha tunadhibiti maambukizi zaidi," alisema King'ori.
Afisa huyo amewataka wakaazi wazingatie kiwango cha juu cha usafi ili kuepuka kuenea kwa ugonjwa huo.