Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Afisa msimamizi wakuwapa wakazi hamasa kuhusiana na masuala ya afya kwenye kaunti ya Nyamira amewaomba wakazi kuhakikisha kuwa wanao wamepata chanjo ya polio, ili kuwaepusha na magonjwa yakupooza.

Akizungumza mjini Nyamira siku ya Jumatatu, Judith Mosomi, aliwasihi wazazi kuhakikisha kuwa wanao wanapata chanjo ili kuwaepusha na maradhi ya kupooza.

Mosomi aliwahimiza wazazi na walezi wa watoto wa umri chini ya miaka kumi na tano na wenye shida yakubeba vitu kutokana na kuwa na mifupa milegevu kutafuta huduma za madaktari haraka.

"Ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha kuwa mwanaye anapata chanjo ya polio ili kuwaepusha watoto dhidi ya maradhi yakupooza. Ikiwa kuna mzazi au mlezi ambaye labda ameona dalili za mtoto wa chini ya miaka kumi na tano kuwa na shida yakubeba vitu, atafute huduma za madaktari haraka. Hali hiyo isiposhughulikiwa kwa haraka, inaweza kuwafanya watoto hao kuwa walemavu," alisema Mosomi.

Afisa huyo aidha aliwasuta wazazi wenye mazoea yakuwapa wanao wenye dalili zakupooza miti shamba, kwa kusema kuwa dawa hizo haziwezi saidia kudhibiti ugonjwa wa polio.

"Ni jambo lakushangaza kuwa kuna wazazi ambao bado wanawapa wanao miti shamba ili kudhibiti ugonjwa wakupooza. Ukweli ni kuwa dawa hizo hazisaidii kwa lolote," alisema Mosomi.