Dereva wawili wa magari ya uma walifikishwa mahakamani siku ya Jumatanao kujibu shtaka la kuendesha gari wakiwa walevi na kuhatarisha maisha ya abiria.
Francis Gachoki na Fanuel Kiarie walifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu James Ogweno. Kiongozi wa mashtaka alieleza mahakama kwamba mnamo Julai 14, 2015 katika barabara la Southern Bypass, eneo la Kikuyu maafisa wa polisi wa idara ya trafiki waliweza kuwatia mbaroni washukiwa hao kwa kudaiwa kuwa walevi wakiwa wamebeba abiria na kuhatarisha maisha yao.
Korti ilielezwa kuwa mshukiwa Gachoki alisimamishwa na afisi wa trafiki mnamo saa nane usiku na kumwamuru kushuke baada ya kugundua kuwa dereva huyo alikuwa mlevi.
Vile vile, kiongozi wa mashtaka aliongeza kuwa polisi walipata pombe aina ya Legend katika mfuko wa sweta ya mshukiwa.
Alipopuliza kifaa cha kudhibitisha kiasi cha ulevi, alipatikana kuwa mlevi kupita kiasi ya kuendesha gari. Alikamatwa na kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kikuyu pamoja na gari hilo.
Alifikishwa mahakamani Jumatano pamoja na chupa ya pombe hiyo ikifikishwa mahakamani kama thibitisho.
Mshukiwa wa pili bwana Kiarie naye mnamo saa tisa akiwa anaendesha gari lililokuwa limebeba abiria katika barabara hilo alidaiwa kuwa mlevi kiasi cha kuhatarisha abiria.
Hata hivyo, wawili hao walikanusha mashtaka dhidi yao. Hakimu Ogweno alihairisha kesi hizo na kusema zitatajwa mnamo Agosti 5, 2015 na kusikizwa Agosti 16, mwaka huu.
Hakimu huyo pia aliwaambia washukiwa hao kuwa wangeendelea na kesi dhidi yao wakiwa nje wakilipa Sh10,000 kila mmoja