Share news tips with us here at Hivisasa

Siku moja tu baada ya vikundi vya vijana kushambuliana kwa mapanga katika mtaa wa Flamingo Nakuru, Mbunge wa Nakuru mjini Samuel Arama ameshtumu swala hilo na kuwataka vijana kudumisha amani. 

Arama anasema kuwa si jambo la busara vijana kujihusisha na machafuko hasa wakati huu tunapoingia katika msimu wa kampeni. 

Ametoa wito kwa vijana wa mitaa ya Kivumbini, Flamingo na Rhonda kudumisha amani. 

"Hii mambo tunaskia Flamingo so nzuri sana na hasa wakati huu wa uchaguzi mkuu ujao, na mimi nawaomba vijana tudumishe amani," alisema Arama. 

Wakati huo huo, ametoa wito kwa idara ya polisi kuimarisha doria katika mitaa hiyo ili kuepuka matukio sawia.