Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria ametoa wito kwa wakuu wa shule za mjini Nakuru kuhakikisha wanadumisha nidhamu miongoni mwa wanafunzi.

Katika mahojiano ya kipekee,mbunge huyo alisema wazazi wanafaa kushirikiana na walimu wa shule hizo kuhakikisha nidhamu miongoni mwa wanafunzi.

"Najua mjini Nakuru kuna shughuli nyingi na kuna umuhimu wa walimu na wazazi kushirikiana ili kuhakikisha watoto hawajiingizi kwa mambo yasiyofaa," Gikaria alisema.

Wakati huo huo mbunge huyo aliongeza kuwa ufanisi hutegemea mwalimu, mzazi na jamii na hivyo basi kuna umuhimu wa ushirikiano.