Hali ya wasiwasi imetanda katika Chuo kikuu cha Anuwai cha Mombasa hii leo, Jumapili baada ya wanafunzi kuskia milio wa risasi karibu na chuo hicho asbuhi na mapema.
Wanafunzi hao walidhani kuwa wamevamiwa na makundi ya kigaidi chuoni humo, na kuanza kutoroka chuoni huku wengine wakitafuta usaidizi kuokoa maisha yao.
Idara ya polisi ata hivyo imesema kuwa milio hiyo ya risasi ilitokana na maafisa waliokuwa wakishika doria waliokuwa wakijaribu kubadilishana zana za kazi bali hakuna uvamizi wowote uliokuwa umetokea.
Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa polisi kisiwani Mombasa Martin Asin alisema kuwa hakuna yeyote amejiyeruhiwa katika kisa hicho, huku akitoa wito kwa wananchi kutoeneza uvumi usiofaa kuhusiana na maswala ya kiusalama.
“Tunawaomba wananchi kuwa wakini na kutoeneza uvumi usiofaa kuhusiana na maswala ya kiusalama, lakini hakuna mtu amejeruhiwa maafisa wetu wa polisi ndio waliyokuwa wakifanya mazoezi karibu na chuo hicho kwa hivyo usalama uko sawa,” alisema Asin.