Serikali imetakiwa kutenga fedha zaidi Kwa IEBC kuelimisha wananchi kuhusu maswala ya kura. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wito huo umetolewa na mwanasiasa Johnson Mwamba Kinyanjui kutoka Njoro, ambaye amesema kuwa idadi ndogo ya wanaojitokeza kusajiliwa ni kutokana na kutoelimishwa. 

"IEBC inafaa kutengewa fedha zaidi ili waweze kuelimisha wananchi kuhusiana na maswala ya kura," alisema Mwamba. Hata hivyo, ametoa wito kwa wakazi wa Njoro kujisajili kwa wingi kama wapiga kura ili kushiriki uchaguzi mkuu ujao. 

Aidha amesema kuwa kwa miaka kadhaa eneo binge la Njoro limesalia nyuma kwani viongozi wanaochaguliwa hawajali maslahi ya mwananchi wa kawaida. 

Mwamba ametangaza azma ya kuwania kiti cha eneo bunge la Njoro katika uchaguzi mkuu ujao mwaka wa 2017.