Naibu gavana wa kaunti ya Kisii Joash Maangi ameshauri jamii ya wakisii kuwajali watoto mayatima na wa familia ambazo hazijiwezi kujiendeleza kimasomo ili kuwazuia watoto hao kujiingiza kwenda mtaani.
Akizungumza mnamo siku ya Jumapili katika eneo la kiamwasi kaunti ya Kisii Maangi aliomba wakisii kuwa katika mstari wa mbele kuwatunza na kuwajali watoto mayatima na wa familia maskini kujiendeleza kimasomo ili kuwazuia kurandaranda mitaani.
“Naomba jamii ya wakisii kujaribu kila iwezalo kuhakikisha kuwa watoto mayatima na wa famila maskini wanaokolewa na kuendelea na masomo yao ili kutorandaranda mitaani,” alisema Maangi.
“Idadi nyingi ya watoto hao katika mitaa mbalimbali ni wale ambao hawana wazazi na familia maskini ambao wamepoteza matumaini ya kuishi vizuri na hata kukosa masomo,” aliongeza Maangi.
Wito huo umetolewa baada ya watoto hao kuongezeka katika mji wa Kisii na wa Nyamira jambo ambalo sasa linatafutiwa suluhu halisi.
Aidha, Maangi alisema serikali ya kaunti ya Kisii kwa ushirikianao na shirika la Nacada wameanzisha kituo katika eneo la Kiamwazi kauti ya Kisii ambacho kitatumika kubadilisha tabia za watoto.