Wananchi wametakiwa kutoilaumu serikali kutokana na utovu wa usalama bali kushirikiana nayo ili kupiga vita makundi ya wahalifu yanayozidi kuchipuka.
Akizungumza na wanahabari ofisini mwake siku ya Jumatatu, Kamishina wa Pwani Nelson Marwa, alisema serikali itawachukulia hatua za kisheria vijana hao licha ya kujali umri wao ikizingatiwa kuwa wengi wa vijana hao ni kati ya umri wa miaka 15-20.
Amewaonya wanasiasa wanaotumia vijana kutatiza usalama wa wakaazi kuwa sheria itawafuata bila ya kujali cheo walichonacho serikalini.
Wakati huo huo amewataka viongozi wa kidini pamoja na wananchi kupeleka majina ya vijana wanaohangaisha wakaazi wa maeneo ya Kisauni kwa mkuu wa usalama katika eneo hilo kama njia ya ushirikiano na idara za usalama kuzuia hali ya utovu wa usalama