Machifu na manaibu wao katika kaunti ya kisii wametishiwa kusimamishwa kazi ikiwa watapatikana wakiruhusu biashara ya pombe haramu kuendelea katika eneo wanalowakilisha.
Hii ni baada ya biashara ya pombe haramu kuonekana kurudiwa tena baada ya kuzimwa kwa mda katika sehemu mbali mbali nchini kutokana na agizo la Rais Uhuru kenyatta.
Akizungumza mjini Kisii kamishena wa kaunti Chege Mwangi alisema chifu na naibu chifu yeyote atakayepatikana akiruhusu pombe haramu katika eneo lake atasimamishwa kazi papo hapo.
“Jambo hili liwaendee machifu na manaibu wao iwapo biashara ya pombe haramu itapatikana katika eneo wanazowakilisha wataenda nyumbani tuachane kiroho safi,” alionya Mwangi.
“Hatutaki biashara ya pombe hiyo kurudiwa tena maana pombe hiyo huadhiri vibaya maisha ya wakazi wengi wanapokunywa,” aliongeza Mwangi.