Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Changamoto imetolewa kwa usimamizi wa kampuni ya sukari ya Kibos iliyoko wilayani Muhoroni kaunti ya Kisumu kuzingatia maslahi ya wenyeji wa eneo hilo inapotekeleza majukumu yake ya kibiashara katika eneo hilo.

Mbunge wa eneo bunge la Muhoroni James Onyango K’Oyoo ametoa wito kwa kampuni ya sukari ya Kibos kuweka utaratibu utakaohakikisha kuwa magari ya kusafirisha miwa hadi kwenye kiwanda hicho hayazui changamoto kama vile vumbi na moshi kwa wenyeji.

Vile vile ameidhibiti kampuni hiyo kudhibiti kelele zinazotokana na mitambo yake akisema kelele hizo huathiri zaidi shuguli za masomo miongoni mwa wanafunzi wanaosoma katika shule za karibu na kiwanda hicho.

Kadhalika, ameshinikiza kampuni hiyo kujali maslahi ya wafanyikazi wao kwa kuchangia katika sekta ya elimu eneo hilo kwa kujenga shule au kupiga jeki masomo kwa kuongeza madarasa zaidi kuwatosheleza wanafunzi.

"Napongeza kampuni ya Kibos kwa juhudi zake za kujiimarisha kiuchumi lakini ni muhimu kuhakikisha kuwa kujiimarisha kwao hakuathiri jamii za karibu na eneo hilo," alisema K’Oyoo.