Serikali ya kaunti ya Nyamira imeunda kamati ya kuhakikisha ufugaji wa ng’ombe na mbuzi wa maziwa umeimarishwa ili kuwanufaisha wafugaji kupitia uuzaji wa maziwa.
Akizungumza siku ya Jumatano mjini Nyamira afisa wa ufugaji katika kaunti ya Nyamira, Alex Migira alisema serikali ya kaunti hiyo imeunda kamati ya kuinua ufugaji wa mifugo katika kaunti hiyo ili kuhakikisha kilimo cha ufugaji kinaimarika zaidi.
“Katika kaunti yetu kuna idadi nyingi ya wafugaji wa ng’ombe na mbuzi lakini hawana njia ya kujifaidi kutokana na mifugo hiyo,” alisema Migira.
“Sisi kama serikali tumeunda kamati ya kuhakikisha wakulima hao wanafaidika kutoka kwa mifugo wao kupitia uzalishaji wa maziwa,” aliongeza Migira.
Pia Migira alisema kuwa tayari serikali hiyo iko na 'Milk coolers' za kuhifadhi maziwa kuzuia kuharibika ili yanapopelekwa kwa mauzo yazipatikane yamearibika
"Kamati ambayo tumeunda ni ya kuangalia mambo hayo na jinsi kilimo cha mifugo kitaimarika zaidi katika kaunti ya Nyamira,” alisema Migira.